KULIPIA BILI ZA MAJI

Posted On: 20th March, 2018

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa IRUWASA inawatangazia wateja wake na wadau wote wa huduma ya maji Iringa kuwa, mwisho wa kulipa bili bila shuruti ni tarehe 28/3/2018. Baada ya tarehe hiyo kupita wateja wote watakaokuwa hawajalipa bili zao za nyuma watasitishiwa huduma. Ili kupata bili yako, tumia simu yako kwa kubonyeza *152*00# Ok. lipa kwa Tigopesa, MPesa, Benki ya NMB na Benki ya Barclays.

Epuka kusitishiwa huduma ya maji, tafadhari lipa bili yako kwa wakati ili Mamlaka iendelee kukuhudumia wewe na mwenzio.