Bibi Doris Ntuli Kalasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa tangu Januari 2024, kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi Ofisi ya Raisi. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 22 katika Utumishi wa Umma akiwa amehudumu katika nyadhifa za mbalimbali za uongozi. Pia aliwahi kufundisha kama Mkufunzi Mgeni katika Taasisi ya Mafunzo ya Wanyamapori ya Pansiasi (Kampasi ya IKOMA, Serengeti, Mkoa wa Mara). Bi. Kalasa ana Shahada ya Uzamili ya Utawala Bora na Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Antwerp, Ubelgiji, na Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.