Serikali kupitia Wizara ya maji na Umwagiliaji kila mwaka huadhimisha wiki ya maji. Madhimisho hayo huenda sambamba na Kaulimbiu ya wiki ya maji Dunian. Kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kote nchini. Kufuatia maadhimisho hayo, shughuli mbalimbali hufanyika zikihusisha Mamlaka za Maji kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali. IRUWASA mwaka huu imeadhimisha wiki ya maji kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo, Upandaji wa miti rafiki ya maji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji, kufanya semina za wafanyakazi, Semina za wadau n.k