News 14th August, 2025
.jpeg)
MKUU WA MKOA WA IRINGA AKAGUA MRADI WA MAJI ISIMANI-KILOLO
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Kheri James leo amefanya ukaguzi wa Mradi wa Maji wa Isimani-Kilolo katika Kijiji cha Holo, mojawapo ya vijiji 29 vinavyonufaika na mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 9.2.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Aidha, amewasihi wananchi kutunza miundombinu ya maji ili mradi huo uendelee kutoa manufaa kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa jukumu la uendelevu wa miradi ya maendeleo ni la kila mwananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Holo nao wameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi huo, wakisema umewaondolea kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji na sasa wana uhakika wa kupata huduma hiyo karibu na makazi yao.
Posted On: 14th August, 2025
News Source: NLUPC Reporters