- Mteja anatakiwa kuwa na vitu vifuatavyo ili kujisajili:
|
- Hati/hati ya Muda (offer) au mkataba wa mauziano wa kisheria.
|
- Picha moja ya rangi ‘‘passport size’’.
|
- Nakala ya kitambulisho cha Mpiga kura au Mkazi au kitambulisho cha Taifa.
|
- Ndani ya siku saba za kazi kuanzia siku aliyofanya maombi ya awali, mteja atapigiwa simu kuja kuchukua makadirio ya gharama za maunganisho.
|
- Mteja ataungiwa maji ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya kukamilisha kufanya malipo (IRUWASA) Kwa kutumia control number utakayopewa.
|
- Mteja akishaunganishiwa maji ataanza kupata bili yake kupitia ujumbe mfupi kwa njia ya simu ya mkononi kwa namba aliyosajili wakati wa kuomba maji.
|