News 21st May, 2025

News Images

BODI YA WAKURUGENZI MAMLAKA YA MAJI MOSHI YATEMBELEA IRUWASA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU

Katika ziara hiyo, wajumbe wa bodi walipata fursa ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya IRUWASA, ikiwemo kituo cha uzalishaji maji cha Ndiuka pamoja na chanzo cha maji cha Kitwiru. Ziara hiyo imelenga kujifunza mbinu mbalimbali za kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza ufanisi wa miundombinu na kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA Mhe Stewart Nkinda alieleza kufurahishwa na namna IRUWASA inavyosimamia shughuli zake, hasa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu ya maji. Aliongeza kuwa ziara hiyo taisaidia bodi yao katika kufanya maamuzi bora ya kimkakati kwa maendeleo ya mamlaka yao.

Mbali na shughuli za kikazi, bodi hiyo pia ilipata nafasi ya kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa, ikiwa ni pamoja na Makumbusho ya Mkwawa yaliyopo Kalenga. Ziara hiyo ya kiutalii ililenga kujionea historia na utamaduni wa Mkoa wa Iringa sambamba na kupumzika baada ya majukumu rasmi.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya IRUWASA Hamid Mohamed Mbata imeeleza kufurahishwa na ziara hiyo na kueleza kuwa hatua hiyo ni ya kupongezwa kwa kuwa inaongeza ushirikiano baina ya mamlaka za maji nchini na kuchochea maendeleo ya pamoja kupitia ubadilishanaji wa uzoefu na maarifa.


Posted On: 21st May, 2025
News Source: NLUPC Reporters