News 16th July, 2025

News Images

MTAALAM MSHAURI TOKA KOREA AENDELEA NA USANIFU MRADI WA MAJI MANISPAA YA IRINGA

Mtaalam Mshauri kutoka kampuni ya KCC ya nchini Korea ameendelea na kazi ya usanifu wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Iringa pamoja na Miji ya Ilula na Kilolo. Hatua hii ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo husika.

Katika kutaka kuelewa hali halisi ya huduma zinazotolewa kwa sasa, Mtaalamu kutoka kampuni ya KCC amefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya IRUWASA. Ziara hiyo imelenga kujionea jinsi huduma ya maji inavyotolewa kwa wananchi pamoja na changamoto zilizopo katika mfumo wa sasa.

Kupitia ziara hiyo, Mtaalamu huyo alitembelea Kidaka maji,Chujio la maji, Chanzo cha maji cha Kitwiru, mtandao wa mabomba pamoja na Kituo cha kusukuma maji Ndiuka, ili kujipatia taarifa halisi zitakazosaidia katika mchakato wa usanifu wa mradi.

Mradi huu unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa huduma bora za majisafi na majitaka kwa wakazi wa Iringa, Ilula na Kilolo hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo hayo


Posted On: 16th July, 2025
News Source: NLUPC Reporters