News 19th November, 2025
BODI YA WAKURUGENZI IRUWASA YAFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA WAFANYAKAZI
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imefanya kikao chake cha kawaida cha mwaka pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka chenye lengo la kusikiliza changamoto, kufanya tathmini ya utendaji kazi na kukumbushana misingi ya utumishi wa umma
Kikao hicho kiliongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Ndugu Edson Elisha Msengi, ambaye aliwahimiza watumishi wa IRUWASA kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Mamlaka inaendelea kuwa taasisi bora ya utoaji huduma za maji nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Ndugu Msengi alisisitiza umuhimu wa watumishi kuongeza juhudi, kushirikiana kwa karibu na kuzingatia maadili ya kazi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Alibainisha kuwa kazi bora na huduma zenye viwango kwa wananchi ni kielelezo cha mafanikio ya IRUWASA.
Katika kikao hicho, wafanyakazi walipata nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao. Bodi pamoja na Menejimenti ya IRUWASA walitoa ufafanuzi na majibu ya changamoto hizo huku wakiahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.
Kikao hikini moja ya vikao muhimu katika kuimarisha mawasiliano baina ya Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi, sambamba na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji
Posted On: 19th November, 2025
News Source: NLUPC Reporters
