News 24th April, 2025

News Images

MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA ZA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MANISPAA YA IRINGA KUANZA KUTEKELEZWA

Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso (Mb.), leo ameshuhudia hafla ya utiaji saini wa mkataba wa usanifu wa mradi wa uboreshaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Iringa pamoja na miji ya Kilolo na Ilula.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Aweso amesisitiza kuwa mradi huo ni wa wananchi na si wa wizara pekee, hivyo ni lazima wananchi washirikishwe kikamilifu katika kila hatua ya utekelezaji wake.

“Nikuombe sana Katibu Mkuu, wizara, na wataalam mliopo hapa mradi huu ambao leo tumeusaini wa zaidi ya shilingi bilioni 275, usiwe mradi wa wizara bali huu ni mradi wa wana Iringa, wananchi wanayo haki ya kujua kila hatua ya utekelezaji. Asije akatokea mtu anataka taarifa ya utekelezaji wa mradi ikasemwa ‘aaah haya ni mambo ya wizara’ jamii ipo na viongozi wapo, ukiwashirikisha utafanikiwa usipowashirikisha utakwama” alisema Waziri Aweso.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amepongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika mkoa wa Iringa.

“Suala la maji taka tuko nyuma sana Iringa ila kwenye water supply tuko mbele 97%, lakini kwenye maji taka ni chini ya 10% hata hivyo, mradi huu in effort za serikali kama ilivyoelekezwa kwenye ilani tunalenga kufikia angalau 30% ya miundombinu ya maji taka.” alisema Mhandisi Waziri.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, amemushukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, hasa katika sekta ya maji, akisisitiza kuwa wananchi wa Iringa wanayo sababu ya kumshukuru kwa kazi kubwa anayofanya.

“Rais Samia kwenye mkoa wetu amefanya kazi kubwa sana, na siyo tu kwenye mradi huu au sekta ya maji kwa kweli kila sekta tumetendewa haki sana. Huu ni mwendelezo wa kazi kubwa anayoifanya. Sisi hapa mjini tumefikiwa na maji 97% lakini ilani ya Chama Cha Mapinduzi ilimtaka afikishe 95% na huko vijijini tumefikia karibu 80% naamini tunapofika mwisho wa mwaka huu, tutakuwa tumefika 85% kulingana na matakwa ya ilani,”

Hata hivyo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ambapo Mkataba huo umesainiwa kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) na mhandisi mshauri kutoka kampuni ya Korea Engineering Consultants Corporation (KECC


Posted On: 24th April, 2025
News Source: NLUPC Reporters