News 1st May, 2025

Mwenge wa Uhuru Wazindua Mradi wa Maji TRM Juu, Iringa – Zaidi ya Wakazi 1,700 Kunufaika
Mradi huu umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali na wadau katika kuhakikisha huduma ya maji inamfikia kila mwananchi, hata wale wanaoishi katika maeneo yenye changamoto za kijiografia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi, aliipongeza IRUWASA kwa kazi nzuri na jitihada madhubuti walizofanya katika kutatua kero ya maji kwa wakazi wa TRM Juu.
"Nawapongeza sana IRUWASA kwa kutekeleza mradi huu kwa ufanisi mkubwa. Huu ni mfano wa taasisi za serikali zinazotekeleza majukumu yake ipasavyo kwa manufaa ya wananchi," alisema Ussi.
Uzinduzi wa mradi huo ni hatua muhimu katika kuimarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo, na ni ishara ya mshikamano kati ya serikali, mamlaka za maji, na jamii katika kupambana na changamoto ya uhaba wa maji nchini.
Posted On: 1st May, 2025
News Source: NLUPC Reporters