News 24th March, 2025

News Images

IRUWASA YATOA SEMINA KWA WADAU KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI 2025

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imefanya semina maalum kwa wadau wake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji 2025. Katika semina hiyo, mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kupitia IRUWASA yaliwasilishwa, yakionyesha hatua kubwa zilizopigwa katika kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Iringa.

Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA Eng. David Pallangyo alieleza mipango ya muda mrefu inayolenga kuboresha zaidi huduma za maji kwa wakazi wa Manispaa hiyo, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa miundombinu na matumizi ya teknolojia za kisasa. Wadau walionesha kuridhishwa na mipango hiyo pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala, wakitoa pongezi kwa juhudi zinazoendelea kufanywa ili kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.


Posted On: 24th March, 2025
News Source: NLUPC Reporters