Dkt. Emilia Mmbando Raila ni mtaalamu anayetambulika kimataifa katika fani za Afya ya Umma, Usimamizi wa Hatari za Mazingira,Mabadiliko ya Tabianchi, na Maji na Usafi wa Mazingira (WASH). Kwa sasa anasimamia utafiti na kuratibu Kituo cha Ubunifu na Ushirikiano wa Jamii (CICE) katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU) tangu Desemba 2025. Dkt. Raila ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 akifanya kazi na mashirika ya kimataifa ikiwemo UNICEF New York, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Ujumbe wa Utulivu wa Umoja wa Mataifa Haiti (MINUSTAH), na UNDP. Amehudumu kama Mshauri Mkuu wa Afya ya Umma na aliongoza mwitikio wa dharura wa WASH wakati wa mlipuko wa Ebola Liberia na tetemeko la ardhi Haiti. Kazi yake imegusa nchi 12 barani Afrika, Asia, na Amerika. Dkt. Raila ana Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Afya ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Walden, USA (2015), Shahada ya Uzamili ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na vyeti vingi vyakitaaluma vya kimataifa.