Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa
(IRUWASA)
Wasifu
Monica Ngezi Mbega photo
Bibi Monica Ngezi Mbega
Mwenyekiti wa Bodi

Wasifu

Bibi Monica Ngenzi Mbega ana taaluma ya usimamizi wa fedha na kiongozi mstaafu katika utumishi wa umma mwenye uzoefu wa miaka 34 katika Utumishi wa Umma, Taasisi za Umma, na Sekta Binafsi. Alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (1995–2010) na Naibu Waziri wa Fedha(1997–1998). Amehudumu katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kilimanjaro (2006–2010). Bibi Mbega amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao (CPB), COASCO, na Shirika la Mbolea Tanzania (TFC), na kwa sasa ni Mjumbe wa Baraza la RUCU na Shule ya Sekondari ya Lugalo.Ana cheti cha Mtaalamu wa Uhasibu (CPA), Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza (2000), na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha (1991).

Mpangilio