Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa
(IRUWASA)
Wasifu
Thadeus John Tenga photo
Mhe. Thadeus John Tenga
Mjumbe wa Bodi-Mwakilishi wa Madiwani

Wasifu

Mhe. Thadeus Tenga ni Diwani wa Kata ya Makorongoni, Manispaa ya Iringa kwa kipindi cha (2025-2030). Kabla ya hapo aliwahi kuhudumu katika nafasi na kata hiyo kwa kipindi cha (2010-2015) na (2020-2025.) Katika baraza la madiwani Manispaa ya Iringa. Mhe Tenga kwa sasa anahudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu. Pia alihudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Makusanyo ya Madini 2012-2015 na Mjumbe wa kamati ya Uchumi, Afya na Elimu. Ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Balozi wa Shina la Makorongoni, Mjumbe wa H/W (2017 – 2022) na Mratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nje ya kazi rasmi alihudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Consolata SACCOS mwaka (2011 – 2020), Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi St. Charles mwaka (2010 – 2020) na Katibu wa kudumu wa Kamati ya usafi na mazingira ya Jimbo Katoliki Iringa. Mhe Tenga ana Taaluma ya Masuala ya Usafifirishaji kutoka Chuo cha Usafifirishaji Tanzania (NIT). Amehudhuria kozi na Mafunzo Mbalimbali kama vile Uongozi wa Familia (M.E). Elimu ya SACCOS na Utunzanji wa hazina na Kozi mbailimbali zaUjasiliamali.

Mpangilio