Bibi Zaina Mfaume Mlawa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa tangu tarehe 23 Juni 2025. Kabla ya nafasi hii, alihudumu kama DED wa Bahi, Mkoa wa Dodoma (Juni 2023–Juni 2025), DED wa Mufindi DC, Mkoa wa Iringa (Novemba 2021–Juni 2023), Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe (Desemba 2016–Novemba 2021), na Katibu wa CCM katika Wilaya za Kilindi na Pangani, Mkoa wa Tanga (2011–2016). Kabla ya hapo, alihudumu kama Mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Mahurunga, Mtwara (2006–2009). Kielimu, ana Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Taaluma za Maendeleo (M.A DS) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Taasisi ya Taaluma za Maendeleo, Shahada ya Kwanza ya Sanaa ya Elimu (Kiingereza na Jiografifia) kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, na Stashahada ya Ualimu kutoka Chuo cha Ualimu Mtwara na ameshiriki katika mafunzo ya uongozi wa maadili, Kozi ya NDC Capstone, na semina za maendeleo Nchini China.