Bibi. Zawadi Gaitan Mgongolwa ni Mwalimu mstaafu katika Utumishi wa Umma, mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30. Katika uzoefu wake wa kazi, alihudumukama Mwakilishi wa CWT (2001–2005), Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake cha CWT (2002–2010), Mwenyekiti wa Wilaya wa CWT (2010–2022), na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mkoa wa Iringa (2010–2022). Alistaafu Utumishi wa Umma kama Mwalimu mwaka 2022, na kwa sasa anajishughulisha na kazi za Ushereheshaji (MC) katika matukio mbalimbali. Bibi Zawadi alishiriki Mafunzo ya Ualimu Daraja "C" katika Chuo cha Ualimu Morogoro. Baadaye alipata Mafunzo ya Ualimu Daraja la 3"A" kutoka Chuo cha Ualimu Klerruu Mkoa wa Iringa. Mafunzo yake mengine ni pamoja na Ualimu wa Kilimo (Songea), Elimu ya Sheria na Haki za Binadamu (Iringa), mafunzo ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), na Lishe Endelevu (Iringa).