Barua pepe: david.pallangyo2@iruwasa.go.tz
Simu: +255754279901
Eng. David Theophil Pallangyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA) tangu Februari2021. Kabla ya uteuzi huu, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) kutoka Septemba 2014 hadi Desemba 2020, na Meneja wa Ufundi wa DUWASA kutoka Agosti 2006 hadi Septemba 2014. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika uhandisi wa usambazaji maji, mipango ya miundombinu, ujenzi, na usimamizi wa huduma za maji. Pallangyo ni Mhandisi Mtaalamu Msajiliwa (Na. 2980) katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Tanzania na mwanachama wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET). Ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Maji na miundombinu ya Manispaa kutoka UNESCO-IHE, Delft, Uholanzi (2007), na Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi wa Kiraia (BSc in Civil Engineering Hons.) kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda (2002).