AUWSA WATEMBELEA IRUWASA KWA LENGO LA KUBADILISHANA UZOEFU
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) wametembelea IRUWASA kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika mbinu mbalimbali zinazotumika katika utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira.
Katika ziara hiyo, watumishi wa AUWSA wamepata fursa ya kutembelea baadhi ya miundombinu muhimu ya IRUWASA ikiwemo Kituo cha Uzalishaji Maji cha Ndiuka, ambapo walijionea hatua mbalimbali za uzalishaji na usambazaji wa majisafi kwa wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Pia wageni hao wametembelea Mabwawa ya Kutibu Majitaka yaliyopo eneo la Don Bosco na kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za usafi wa mazingira .
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Taasisi za maji nchini kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na maendeleo ya sekta ya majisafi na usafi wa mazingira nchini.