WCF WATOA ELIMU KWA WATUMISHI WA IRUWASA
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendesha semina kwa watumishi wa IRUWASA kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu majukumu, huduma na stahiki mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo kwa wafanyakazi wanapopata madhara yatokanayo na kazi.
Kupitia semina hiyo, watumishi wamepata fursa ya kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu WCF, ikiwemo haki zao, taratibu za kupata fidia na hatua zinazopaswa kufuatwa pale mfanyakazi anapopata ajali, ugonjwa au madhara mengine yanayotokana na mazingira ya kazi.
Semina hiyo inalenga kuongeza uelewa kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kuwahamasisha kufahamu stahiki zao na kuhakikisha wanatumia fursa na huduma zinazotolewa na WCF kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.