WATUMISHI WA IRUWASA WAPATIWA MAFUNZO YA AFYA YA AKILI, UNYANYASAJI WA KIJINSIA NA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) wamepata mafunzo kuhusu afya ya akili, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa afya ya akili na ustawi wa watumishi katika mazingira ya kazi na maisha ya kila siku. Mafunzo haya yametolewa na Dkt. Garvin Kweka, daktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kituo cha Iringa. Katika mafu...