News 15th February, 2024

News Images

IRUWASA NAMBA MBILI KUSINI NA MASHARIKI MWA BARA LA AFRIKA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa IRUWASA imefanikiwa kuibuka mshindi wa pili kati ya Mamlaka za Maji za Kusini na Mashariki Mwa Afrika.

Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Wadhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAWAS) ambayo hushindanisha Mamlaka ambazo zinazofanya vizuri Kusini mashariki mwa Afrika, imetoa takwimu zake na IRUWASA kuibuka mshindi wa pili kati ya Mamlaka bora Kusini n Mashariki mwa Africa.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo Mamlaka zilizofanya vizuri ni Nyeri Kenya, IRUWASA Tanzania, WASAC Rwanda, EWSC Zambia na BWB Malawi.


Posted On: 15th February, 2024
News Source: NLUPC Reporters