News 14th May, 2024

IRUWASA YAPELEKA NEEMA KATA YA MLAFU
MAMLAKA ya maji na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) imeingia mkataba na kampuni ya Intercecon LTD kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kata ya Mlafu iliyo halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoa wa IRINGA.
Mradi huu unalenga kuwafikia zaidi ya wananchi 7000 na unagharimu zaidi Bilioni 1.3 na utatekelezwa kwa siku 365 sawa na Mwaka Mmoja.
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza adha ya muda Mrefu waliyokuwa wakipitia wakazi hao kwakutopata huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 60 ya Uhuru
Posted On: 14th May, 2024
News Source: NLUPC Reporters