News 15th June, 2026
BODI MPYA YA IRUWASA YAKUTANA NA WATUMISHI
Bodi ya 10 ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA) imefanya kikao na Watumishi katika kikao maalum kilicholenga kufahamiana na kujenga ushirikiano wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi, Monica Ngenzi Mbega, alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji kwa kila Mtumishi ili kuhakikisha huduma bora za maji na usafi wa mazingira zinaendelea kutolewa kwa wananchi wa Iringa.
Bi Mbega alisema kuwa mafanikio ya IRUWASA yanategemea mshikamano, nidhamu ya kazi na kujituma kwa kila Mtumishi katika kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi. Aidha, aliwahimiza Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana na kudumisha maadili ya utumishi wa umma ili kuongeza kiwango cha huduma na kuridhisha wateja wa IRUWASA.
Kwa upande, Watumishi walipata fursa ya kuijua Bodi mpya na kubadilishana mawazo kuhusu namna bora ya kuimarisha utendaji kazi na kufanikisha malengo ya IRUWASA katika kuwahudumia wananchi.
Posted On: 15th June, 2026
News Source: NLUPC Reporters
