News 21st March, 2024

IRUWASA NAMBA MOJA TANZANIA
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Iringa IRUWASA, Imefanikiwa kuibuka wa kwanza kati ya mamlaka za maji Tanzania kwa kutoa huduma bora za majisafi na usafi wa mazingira
Tuzo hiyo ambayo hutolewa na EWURA kila mwaka Katika kuthamini utendaji wa mamlaka za maji zinazofanya vizuri zaidi kwa kuangalia kiwango na muda wa upatikanaji wa maji katika eneo husika, kiwango cha maji yanapotea na huduma ya uondoshaji majita taka..
Kupitia vigezo hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeitangaza IRUWASA kuwa mamlaka ya kwanza kati ya mamlaka 26 za miji mikuu ya mikoa nchini kwa utoaji wa huduma za maji safi na uondoshaji wa maji taka kwa mwaka 2022/2023.
Posted On: 21st March, 2024
News Source: NLUPC Reporters