News 30th September, 2023
IRUWASA YAPANDA DARAJA, MKURUGENZI PALLANGYO ATOA NENO
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo amesema kupanda kwa mamlaka hadi kufikia daraja AA ni ishara kuwa iruwasa inafanya vizuri katika kuwahudumia wananchi.
Kauli hiyo Mhandisi Pallangyo ameitoa Septemba jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya Bodi na Menejimenti za Mamlaka za Maji Tanzania Bara ambapo IRUWASA ni miongoni mwa Mamlaka zilizopandishwa madaraja
Posted On: 30th September, 2023
News Source: NLUPC Reporters