News 15th October, 2024
IRUWASA YATAMBULIWA KWA USHIRIKIANO MZURI NA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA
Katika kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, IRUWASA yatambuliwa kwa ushirikiano mzuri kati yake na Shirika la Bima la Taifa (NIC). Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA eng. David Pallangyo, akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Shirika hilo kama ishara ya kuonesha ushirikiano mzuri kati ya Taasisi hizi mbili.
Aidha, kwa upande mwingine IRUWASA imekuwa ni Taasisi ya mfano kwa utoaji wa huduma Bora za Majisafi na Usafi wa mazingira Nchini. Kudhihiridha hili, mnamo mwezi Septemba 2024, ESAWAS iliitangaza IRUWASA kushika nafasi ya pili kati ya Mamlaka za Maji za Nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika kwa mwaka 2022/2023 ikitanguliwa Mamlaka ya Maji Nakuru iliyoko Nchini Kenya iliyoshika namba moja.
IRUWASA imejipanga kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kusimamia kwa karibu huduma inazozitoa ili kuwahakikishia wananchi huduma bora na endelevu za Majisafi na Usafi wa mazingira muda wote
Posted On: 15th October, 2024
News Source: NLUPC Reporters