News 8th July, 2025

News Images

Wanafunzi wa Ruaha Catholic University Wabuni Mita ya Maji ya Malipo ya Kabla

Katika wasilisho hilo, mwanafunzi Elibarick Marcel alieleza kuwa wazo la kuunda mita hiyo lilitokana na changamoto wanazokumbana nazo kama wanafunzi wanaoishi kwenye nyumba za kupanga, ambapo mara kwa mara hukutana na matatizo ya malipo ya maji. “Changamoto hizo ndizo zilizotusukuma kutafuta suluhisho la kiteknolojia ambalo litawezesha wateja kulipia maji kabla ya matumizi,” alisema Marcel.

Mwalimu wa wanafunzi hao, Bw. Abdallah Haji, alitumia fursa hiyo kuwaalika wadau wa sekta ya maji na teknolojia kuwekeza kwenye miradi ya ubunifu ya wanafunzi kwa lengo la kukuza soko la ajira na kuendeleza maarifa ya kiteknolojia miongoni mwa vijana.

Kwa upande wake, Meneja wa Bili na Madeni kutoka IRUWASA, Bw. Oscar Salingwa, aliwapongeza wanafunzi hao kwa wazo lao la kibunifu na kuwataka wasichoke kuboresha kifaa hicho ili kiweze kutumika rasmi katika kutatua changamoto mbalimbali za bili za wateja.

Ubunifu huo umeonekana kuwa na matumaini makubwa katika kuboresha huduma za maji kwa kurahisisha mfumo wa malipo na kudhibiti matumizi, huku ukichangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza migogoro kati ya wapangaji na wamiliki wa nyumba.


Posted On: 8th July, 2025
News Source: NLUPC Reporters