News 27th April, 2026

News Images

IRUWASA YAZINDUA BODI YA 10 YA WAKURUGENZI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA) limezindua rasmi Bodi yake ya Kumi ya Wakurugenzi katika hafla iliyofanyika tarehe 24 Aprili 2026 kwenye ukumbi wa Masiti Hall, mkoani Iringa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Benjamini Sitta, sambamba na wageni wengine waalikwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, aliipongeza IRUWASA kwa juhudi zake katika kuboresha huduma za maji kwa wananchi. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia weledi, uwajibikaji na mahitaji ya wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mha. Mwajuma Waziri, alihimiza IRUWASA kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia, hususan kwa kufunga mita za malipo ya kabla (Prepaid meters) kwa wateja wapya. Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kufikia lengo la wizara la kuhakikisha wananchi wote wanaotumia huduma ya maji wanatumia mfumo wa malipo ya kabla. “Bodi hii iende ikaache Legacy kwa kuhakikisha inaondoa “Postpaid” mita na kufunga prepaid meter ili wananchi waweze kuipa bili kwa wakati kuepukana na suala la madeni”. Alisema Mhadisi waziri.

Uzinduzi wa bodi hiI mpya unatarajiwa kuimarisha uongozi na usimamizi wa IRUWASA, pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa mkoa wa Iringa.


Posted On: 27th April, 2026
News Source: NLUPC Reporters