News 20th March, 2018

Utendaji kazi unaozingatia sheria na taratibu
Wafanyakazi wa IRUWASA wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesera alipokuwa akifungua mafunzo ya Wadau wa IRUWASA wakati wa uzinduzi wa maazimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa IRUWASA siku ya tarehe 16/03/2018.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Iringa, mbali na kusisitiza utendaji kazi unaozingatia sheria na taratibu, aliwaasa pia Watumishi wa IRUWASA kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Iringa wanaendelea kupata huduma stahiki za majisafi na usafi wa mazingira.
Aliwasisitiza wananchi wa Iringa kutimiza wajibu wao ikiwemo kulipia huduma hizo kwa wakati ili kufanya huduma hizo kuwa endelevu.
Mhe. Kasesera aliisifu Menejimenti ya IRUWASA kwa namna ilivyojipanga kuhakikisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira Iringa zinaendelea kutolewa kwa wananchi
Posted On: 20th March, 2018
News Source: NLUPC Reporters